Wanachama Sita Wa Green World Ziarani China

 

watanzania ziarani china 2016 mei 19

 

 

Kampuni ya Green World ina viwanda vyake viwili vya kutengeneza bidhaa zinazotokana na mimiea huko nchini China. Viwanda hivyo viwili vipo katika miji ya Nanjing na Tianjin. Viwanda katika miji hiyo hutengeneza bidhaa baada ya matokeo ya utafiti unaofanyika katika vyuo vikuu vya huko Marekani. Moja ya vyuo vikuu hivyo ambavyo ni vituo vya utafiti ni Cornell University ambako muasisi wa kampuni hii, Dr Deming Li, alihitimu masomo yake katika fani ya microbiology na kupata shahada ya uzamifu.

Katika siku za karibuni, kampuni ya Green World imeanza kutengeneza bidhaa zinazotokana na mmea wa strawberry katika kiwanda chake cha mjini Nanjing. Pia kampuni imeanza kutengeneza mbolea itokanayo na viumbe hai, Green World Nutriplant Organic Fertilizer, katika kiwanda chake cha mji huo.

 

hilda wa green world ziarani china

 

Baada ya ufanisi mkubwa wa bidhaa za strawberry, kampuni imeandaa tamasha kusherehekea mafanikio hayo.

Kufanikisha na kuwanufaisha pia wanachama wa kampuni hiyo walio nje ya China, kampuni imawalika wanachama wake kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kuhudhuria tamasha hilo. Wanachama hao watapewa pia fursa ya kutembelea mji wa Shanghai, sehemu za kununua bidhaa za kibiashara na za utalii za mji wa Nanjing.

 

ziara ya china

Wana-Green World Wakiwa Kwenye Uwanja Wa Ndege DSM Kabla Ya Kuondoka Mei 19 2019

 

Nchi ya Tanzania imepewa mwaliko huo na wanachama 6 waliondoka nchini tarehe 19 Mei 2016 kuungana na wenzao wa mataifa mbalimbali. Wanachama wa Green world walioondoka siku hiyo walikuwa ni Scholastica Gwayde, Cecilia Mosha, Martha Tluway, Geofrey Alal, Hilda Mahende, Hanisha Semfuko na Dr. Highness Kaira.

 

wana-green world china mei 19 2016
Baada ya kutembelea sehemu za biashara, kiutalii na kuhudhuria tamasha hilo, wanachama hao wanategemewa kurudi nchini tarehe 27 mei 2016.

 

ziara ya watanzania china mei 19 2016

 
Usisite kutoa maoni au kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu mada hii. Tutafurahi kuona kuwa tumekujibu kwa wakati na kwa ufasaha.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 
Laurian.