Watanzania Washiriki Sherehe Za Miaka 10 Ya Green World, Kenya

 

 

sherehe kenya 1

 

Jiji la Nairobi lilitikisika siku ya jumamosi, tarehe 2 Juni 2018, siku ambayo sherehe kubwa ya kutimiza miaka 10 ya Green World, Kenya ilifanyika. Sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kenyetta International Conferernce Centre, ndani ya ukumbi wa Tsavo Ballroom.

Sherehe zilianza saa 3.00 asubuhi na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika walishiriki. Sherehe zilianza kwa maandamano ya kuzunguka mjini Nairobi zikiongozwa na matarumbeta. Baadaye wanachama walirudi katika ukumbi na matukio mbali mbali yaliendelea kwa mpangilio makini.

Washiriki walitoka nchini Afrika Kusini, wakiongozwa na mama Thembi, kutoka Zimbabwe wakiongozwa na ndugu Tendai. Washiriki wengi pia walitoka Nigeria. Wengine walitoka Uganda, Msumbiji, mmoja alitoka Ruanda. Watanzania walioongozwa na ndugu Gaudence Mbuya walikuwa, Mrs Mbuya, hawa (mtu na mkewe) walitoka Arusha. Ndugu Sofia pia wa Arusha alishiriki. Ndugu Mashaka Mabele alitoka Mwanza, ndugu Laurian Mwajombe na dada Hilda Mahende wao walitoka Dar Es Salaam.

 

sherehe za nairobi
Katika sherehe hizo, zawadi mbalimbali zilitolewa, pamoja na magari 26 yaliyokwenda kwa wanachama wa Kenya, kila gari likiwa na thamani ya Tshs milioni 20. Zawadi za safari za nje pia zilitolewa. Kulikuwepo na bahati nasibu ya papo kwa hapo ambapo zawadi nyngi zikiwemo smart phones zilitolewa.

 

shereh kenya 2

 

Wasemaji wakuu katika sherehe hiyo walikuwa ndugu David Zhang, raisi wa Green World Afrika, ndugu Tendai Chinoperekwei wa Zimbabwe (1* Director), mama Lucy Miano wa Kenya (3*manager), Steven Mbogo wa Kenya (8* Consultant) na wengineo.

Sherehe ziliisha mnamo saa 11 na kufungwa kwa sala maalumu.

Kuona kipande cha video cha sherehe hizo bofya juu ya picha hapa chini:

 

video ya sherehe za kenya

 

Kuifahama zaidi kampuni ya Green World, pitia ukurasa huu:  http://biasharayamtandao.sagalawebs.com/

 

Laurian.