Yahusu BV Za Wanachama

 

office mpya ya Green World

 

Tunapenda kutoa maelezo kidogo kuhusu hali iliyojitokeza ya wanachama kushindwa kuingia kwenye tovuti ya kampuni na kuona BV zao. Ni kitu ambacho kimeanzia kwenye makao makuu ya kampuni  kutokana na kufungwa rasmi kwa tawi la Green World Tanzania.

Tayari tumewasliana na ofisi ya Nairobi na wametuahidi kuwasiliana na makao makuu ili suala hili liweze kurekebishwa. Tutalifuatlia kwa ukaribu na kutoa maendeleo kila wakati.

Wanachama mnaombwa kuhudhuria mafunzo ambayo tayari yameanza ofisini  hapa Karume. Ratiba ni ile ile ya siku za jumanne, alhamisi na jumamosi. Bila mafunzo na mijadala baina yetu maendeleo yatakuwa kidogo sana.

Binafsi naona uchungu sana ninapoona wanachama wanahangaika na maisha wakati wenzetu ni matajiri kupitia fursa hii hii ya Green World.

 

Laurian.