Jumamosi ya tarehe 19 Novemba 2017, mji na wakazi wa mji wa Johannesburg walishuhudia mtingishiko uliotokana na shamra shamra za wanachama wa kampuni ya Green World waliofika humo kutoka pande zote za dunia, Wanachama walianza kufurika mjini hapo asubuhi ya siku ya ijumaa na wote walipokelewa na kusalimiwa mmoja baada ya mwingine na mwanzilishi na rais wa kampuni hiyo, ndugu Prof Deming Li. Wanachama waliongozwa hadi kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota 5 iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili yao.
Siku ya jumamosi wanachama walianza kuingia kwenye ukumbi wa Ellis Park Indoor Arena muda wa saa 4 asubuhi na kufikia saa 6 sherehe zilianza rasmi. Ukumbi ulifurika ukiwa na wanachama zaidi ya elfu nne kutoka nchi zaidi ya 70 duniani.
Sherehe zilianza kwa kuwakaribisha wale waliofuzu kufika nchini humo baada ya kukidhi matakwa ya promosheni iliyotolewa, vikiwemo vipindi vya wasemaji kutoka chi mbalimbali na baadaye hotuba kutoka kwa Prof Deming Li mwenyewe. Alieleza kuwa kampuni inafanya jitihada za kuwawezesha wanachma kuifanya biashara yao kupitia njia za kisasa ikiwemo njia ya mtandao. Alitaarifu kuwa kuna app ambayo imetayarishwa mahsusi kwa ajili ya kampuni ya Green world na muda si mfupi itatolewa na kupatikana Google Store.
Wanachama mbalimbali baadaye walipewa zawadi zao za utendaji bora, yakiwemo mamia ya magari madogo, magari ya kifahari yapatayo 38, villa moja. Vigelegele na nderemo vilifunika ukumbi pale ndugu Tendai wa Zimbabwe alipokabidhiwa daraja jipya la 1*M (One Star mManager) na mama Thembi Ngidi wa Afrika ya Kusini kukabidhiwa daraja la 2*M.
Katika sherehe hiyo , Tanzania iliwakilishwa vilivyo na ndugu Gaudens Mbuya na mkewe Agnes kwa kila mmoja kupata gari ndogo moja ya biashara.