Pamoja na bidhaa za kulinda afya ya binadamu, kampuni ya Green World inatengeneza na kusambaza mbolea ya aina mpya inayotokana na mabaki ya viumbe hai. Madhumini ya kutengeneza aina hii ya mbolea ni kumlinda binadamu kutokana na kemikali za mbolea za Inorganic Fertilizers. Mbolea hiyo pamoja na kuwa na viambato vyote vinavyohitajika kwa wingi katika ustawi wa mimea (macronutrients), ina viambato vingi vinavyohitajika wa kiwango kidogo (micronutrients). Kwa kufahamu kuwa mimea huhitaji amino-acids, mbolea hii imejumuisha aina 18 tofauti za amino-acids ndani yake.
Kufahamu undani wa mbolea hii, unaweza kusoma hapa: http://topantiagingproducts.sagalawebs.com/mbolea-ya-green-world-green-world-nutriplant-organic-plus-fertilizer/
Nchi kadhaa za barani Afrika zimeikubali mbolea hii baada ya wizara husika za nchi hizo kuipeleka mbolea hii kwenye maabara zao, kuifanyia vipimo na kubaini kuwa inakidhi viwangi vinavyohitajika. Nchi hizi ni pamoja na Nigeria.
Baada ya kupita kwenye maabara za hapa nchini Tanzania, hatimaye mbolea hii imekubalika na kupewa usajili rasmi na Tanzania Fertilizer Regulatory Authority (TFRA). Mbolea hii imesajiliwa kwa jina la Nutriplant Organic Plus Fertilizer tarehe 18/09/2017 na kupewa usajili namba 0239.
Tunawashauri watanzania kuanza kuiutumia mbolea hii kwani ina faida nyingi zaidi ya zile zinazopatikana kwenye mbolea nyingine tulizozizoea za kufukia ardhini. Faida ya zaidi ya kuongeza uwingi na ubora wa mazao yako, mbolea hii huiboresha ardhi yako badala ya kuiharibu kama ilivyo kwa mbolea nyingine.