Watanzania Washiriki Sherehe Za Miaka 10 Ya Green World, Kenya

 

 

sherehe kenya 1

 

Jiji la Nairobi lilitikisika siku ya jumamosi, tarehe 2 Juni 2018, siku ambayo sherehe kubwa ya kutimiza miaka 10 ya Green World, Kenya ilifanyika. Sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kenyetta International Conferernce Centre, ndani ya ukumbi wa Tsavo Ballroom.

Sherehe zilianza saa 3.00 asubuhi na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika walishiriki. Sherehe zilianza kwa maandamano ya kuzunguka mjini Nairobi zikiongozwa na matarumbeta. Baadaye wanachama walirudi katika ukumbi na matukio mbali mbali yaliendelea kwa mpangilio makini.

Washiriki walitoka nchini Afrika Kusini, wakiongozwa na mama Thembi, kutoka Zimbabwe wakiongozwa na ndugu Tendai. Washiriki wengi pia walitoka Nigeria. Wengine walitoka Uganda, Msumbiji, mmoja alitoka Ruanda. Watanzania walioongozwa na ndugu Gaudence Mbuya walikuwa, Mrs Mbuya, hawa (mtu na mkewe) walitoka Arusha. Ndugu Sofia pia wa Arusha alishiriki. Ndugu Mashaka Mabele alitoka Mwanza, ndugu Laurian Mwajombe na dada Hilda Mahende wao walitoka Dar Es Salaam.

 

sherehe za nairobi
Katika sherehe hizo, zawadi mbalimbali zilitolewa, pamoja na magari 26 yaliyokwenda kwa wanachama wa Kenya, kila gari likiwa na thamani ya Tshs milioni 20. Zawadi za safari za nje pia zilitolewa. Kulikuwepo na bahati nasibu ya papo kwa hapo ambapo zawadi nyngi zikiwemo smart phones zilitolewa.

 

shereh kenya 2

 

Wasemaji wakuu katika sherehe hiyo walikuwa ndugu David Zhang, raisi wa Green World Afrika, ndugu Tendai Chinoperekwei wa Zimbabwe (1* Director), mama Lucy Miano wa Kenya (3*manager), Steven Mbogo wa Kenya (8* Consultant) na wengineo.

Sherehe ziliisha mnamo saa 11 na kufungwa kwa sala maalumu.

Kuona kipande cha video cha sherehe hizo bofya juu ya picha hapa chini:

 

video ya sherehe za kenya

 

Kuifahama zaidi kampuni ya Green World, pitia ukurasa huu:  http://biasharayamtandao.sagalawebs.com/

 

Laurian.

Timu T029 Yahamishiwa Nairobi

 

IT Room - Nairobi office

CHUMBA CHA IT NDANI YA OFISI YA GREEN WORLD YA NAIROBI

 

Baada ya ofisi ya kampuni ya Green World kufungwa hapa Dar es salaam – Tanzania, shughuli za kampuni hiyo zinaendelea kupitia maduka ya wanachama. Wanachama hao wenye maduka waliamua kuendesha shughuli zao sehemu tofauti.  Wakati wengine walichagua kwenda  Lusaka – Zambia, wengine walielekea Nairobi – Kenya.

Timu nzima inayopata huduma kutoka duka T029 imehamishiwa Nairobi, maana yake ni kwamba BV za members wa duka hilo zitapelekwa huko kila mwezi na bonasi zitapatikana kutoka ofisi hiyo ya Nairobi. Ili kuona shughuli zako za kibiashara, kuna mabadiliko kidogo katika ku-login kwenye page yako. Pata maelekezo kamili kutoka link hiyo hapo chini:

N.B. Badala ya TZ01 andika KE01

 

http://topantiagingproducts.sagalawebs.com/namna-ya-kuingia-kwenye-tovuti-yako-ya-green-world/

 

Kwa mara ya kwanza kupitia utaratibu huu, bonasi za desemba 2017 zimepatikana kutoka Nairobi.

Laurian.

                WE CARE   WE SHARE

 

 

Mabadiliko Ya Bei Ya Bidhaa Za Green World

 

Moja ya maduka ya Green World linafanya kazi zake kupitia ofisi ya Green World ya Nairobi, Kenya. Duka hili limewajibika kubadilisha bei ya bidhaa za kampuni hapa kwetu kutokana na kuwa thamani za shilingi ya Kenya na Tanzania kwa dola zinatofautiana na kwa kuwa shilingi moja ya Kenya inauzwa kwa wastani wa shilingi 22 za Tanzania.

 

Bei Nov 2017

 

Mabadiliko haya ya bei yanaanza tarehe mosi Novemba 2017.

Ofisi ipo katika harakati ya kubadilisha nyaraka nyingine nyingi za kufanyia kazi. Mategemeo ni kuwa kila kitu kitakuwa sawa hadi kufika mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba.

GO GREEN    GO SUCCESS.

Yahusu BV Za Wanachama

 

office mpya ya Green World

 

Tunapenda kutoa maelezo kidogo kuhusu hali iliyojitokeza ya wanachama kushindwa kuingia kwenye tovuti ya kampuni na kuona BV zao. Ni kitu ambacho kimeanzia kwenye makao makuu ya kampuni  kutokana na kufungwa rasmi kwa tawi la Green World Tanzania.

Tayari tumewasliana na ofisi ya Nairobi na wametuahidi kuwasiliana na makao makuu ili suala hili liweze kurekebishwa. Tutalifuatlia kwa ukaribu na kutoa maendeleo kila wakati.

Wanachama mnaombwa kuhudhuria mafunzo ambayo tayari yameanza ofisini  hapa Karume. Ratiba ni ile ile ya siku za jumanne, alhamisi na jumamosi. Bila mafunzo na mijadala baina yetu maendeleo yatakuwa kidogo sana.

Binafsi naona uchungu sana ninapoona wanachama wanahangaika na maisha wakati wenzetu ni matajiri kupitia fursa hii hii ya Green World.

 

Laurian.

SHEREHE ZA GREEN WORLD – AFRIKA YA KUSINI

 

IMG-20171119-WA0014

 

Jumamosi ya tarehe 19 Novemba 2017, mji na wakazi wa mji wa Johannesburg walishuhudia mtingishiko uliotokana na shamra shamra za wanachama wa kampuni ya Green World waliofika humo kutoka pande zote za dunia, Wanachama walianza kufurika mjini hapo asubuhi ya siku ya ijumaa na wote walipokelewa na kusalimiwa mmoja baada ya mwingine na mwanzilishi na rais wa kampuni hiyo, ndugu Prof Deming Li. Wanachama waliongozwa hadi kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota 5 iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili yao.

Siku ya jumamosi wanachama walianza kuingia kwenye ukumbi wa Ellis Park Indoor Arena muda wa saa 4 asubuhi na kufikia saa 6 sherehe zilianza rasmi. Ukumbi ulifurika ukiwa na wanachama zaidi ya elfu nne kutoka nchi zaidi ya 70 duniani.

 

IMG-20171119-WA0031

Sherehe zilianza kwa kuwakaribisha wale waliofuzu kufika nchini humo baada ya kukidhi matakwa ya promosheni iliyotolewa, vikiwemo vipindi vya wasemaji kutoka chi mbalimbali na baadaye hotuba kutoka kwa Prof Deming Li mwenyewe. Alieleza kuwa kampuni inafanya jitihada za kuwawezesha wanachma kuifanya biashara yao kupitia njia za kisasa ikiwemo njia ya mtandao. Alitaarifu kuwa kuna app ambayo imetayarishwa mahsusi kwa ajili ya kampuni ya Green world na muda si mfupi itatolewa na kupatikana Google Store.

 

IMG-20171119-WA0042

 

Wanachama mbalimbali baadaye walipewa zawadi zao za utendaji bora, yakiwemo mamia ya magari madogo, magari ya kifahari yapatayo 38, villa moja. Vigelegele na nderemo vilifunika ukumbi pale ndugu Tendai wa Zimbabwe alipokabidhiwa daraja jipya la 1*M (One Star mManager) na mama Thembi Ngidi wa Afrika ya Kusini kukabidhiwa daraja la 2*M.

 

IMG-20171119-WA0040

 

Katika sherehe hiyo , Tanzania iliwakilishwa vilivyo na ndugu Gaudens Mbuya na mkewe Agnes kwa kila mmoja kupata gari ndogo moja ya biashara.

Mabadiliko Ya Uongozi Wa Green World

 

 

machinga complex office

 

Historia

Mnamo wiki mbili za mwisho za mwezi Oktoba 2017, Meneja wa Green World Tanzania Branch alitutaarifu wanachama tunaoishi Dar Es Salaam kuwa ofisi ya Green World inatakiwa ifungwe katika siku 3 na kwamba tayari taratibu za kuuza samani za kampuni zilikuwa zimeanza. Sababu halisi za kufungwa kwa ofisi hazikufafanuliwa. Na hadi kufika Novemba mosi, hapakuwepo shughuli zo zote za kiofisi.

Baadaye meneja aliandaa kikao cha watu wachache na kueleza kuwa shughuli za kampuni zitaendeshwa kupitia maduka (shops) zilizopo ambazo moja ipo Mwenge, nyingine Arusha, Tabata, Makumbusho na Karume (Machinga Complex Building). Na ili kupata bidhaa na bonasi za wanachama, meneja alitushauri maduka hayo kuchagua kufanya kazi kutoka Nairobi, Lusaka au Kampala.

Kilichofanyika

Baada ya kauli hizo za meneja wetu, baadhi ya wenye maduka walienda Lusaka na wengine Nairobi ili kukamilisha taratibu za kuagiza mizigo na kupata bonasi za wanachama.

Kwenye ukurasa huu, nitazungumzia kilichofanyika kwa duka namba T029 ambalo linamilikiwa na mwanachama ndugu Laurian Mwajombe.

Ndugu Laurian Mwajombe alielekea Nairobi ili kukutana na uongozi wa huko ambako alipata mwongozo mkubwa kutoka kwa ndugu Lucy (Green World 3* Manager). Akiwa huko alifika makao makuu ya Green World Nairobi na kupata mwongozo wa jinsi ya kuagiza bidhaa, kupata bonasi za wanachama wa duka namba T029, orodha na bei za bidhaa zilizopo na mengineyo mengi ya msingi.

Yatokanayo

1. Taratibu za Kenya zinahitaji mauzo yafanyike mwisho tarehe 30 au 31 ya kila mwezi. Kwa mantiki hiyo, kwetu hapa Tanzania, mauzo yafanyike mwisho tarehe 27 ya mwezi ili kupata muda wa kuandaa na kupeleka marejesho Nairobi.

2. Bonasi zitatumwa kila tarehe 20 ya mwezi.

3. Wanachama ambao hawapo ndani ya T029, ili waweze kupata bonasi zao kutoka Nairobi kama watapenda kufanya hivyo, watapaswa kutoa maombi yao na yatapelekwa Nairobi.

3. Kunaweza kukatokea mabadiliko kidogo katika bei ya bidhaa kutokana na tofauti za pesa za Tanzania na Kenya.

4. Bonasi za mwezi huu hazitaweza kutolewa kwa sababu ya kuchelewa kuziwasilisha Nairobi. Lakini BV zote hazipotei, badala yake zitaunganishwa na za mwezi huu na bonasi ya jumla kutolewa tarehe 20 ya mwezi ujao.

5. Duka letu lipo Karume ndani ya jengo la Machinga Complex. Tupo ghorofa ya 3 karibu na ofisi za DRFA (Dar Es Salaam Region Football Association).

6. Wanachama wapya watapata kadi zao kutoka Nairobi. Itachukua muda kidogo kupata kadi zao na start kit zao kwani zitaletwa pale tutakapokuwa tumeagiza products.

7. Itachukua muda kidogo kupata fomu za manunuzi na za  kuunganisha wanachama wapya kwani gharama hizi zote ni kwa mwenye duka.

8. Sasa hivi ofisi ya Kenya haitoi zawadi ndogo. Zawadi hizi ni za 3*C , 4*C na 5*C katika mwezi mmoja. Wanaanzia zawadi ya 6*C katika miezi 6 (Tripu ya China).

Mwisho

Tunaomba wanachamma kuwa watulivu na kusoma maelezo haya kwa kina na kuyatafakari. Kama kuna maswali, usisite kuyauliza. Tunakuomba kwa kipindi hiki cha mwanzo kutunza BV vizuri zako na kuzifuatilia kutoka kwenye tovuti ya kampuni.

 

Laurian

Mbolea ya Green World Yapata Usajili

 

ubora wa mazao na green world

Pamoja na bidhaa za kulinda afya ya binadamu, kampuni ya Green World inatengeneza na kusambaza mbolea ya aina mpya inayotokana na mabaki ya viumbe hai. Madhumini ya kutengeneza aina hii ya mbolea ni kumlinda binadamu kutokana na kemikali za mbolea za Inorganic Fertilizers. Mbolea hiyo pamoja na kuwa na viambato vyote vinavyohitajika kwa wingi katika ustawi wa mimea (macronutrients), ina viambato vingi vinavyohitajika wa kiwango kidogo (micronutrients). Kwa kufahamu kuwa mimea huhitaji amino-acids, mbolea hii imejumuisha aina 18 tofauti za amino-acids ndani yake.

Kufahamu undani wa mbolea hii, unaweza kusoma hapa:  http://topantiagingproducts.sagalawebs.com/mbolea-ya-green-world-green-world-nutriplant-organic-plus-fertilizer/

 

Nchi kadhaa za barani Afrika zimeikubali mbolea hii baada ya wizara husika za nchi hizo kuipeleka mbolea hii kwenye maabara zao, kuifanyia vipimo na kubaini kuwa inakidhi viwangi vinavyohitajika. Nchi hizi ni pamoja na Nigeria.

 

 

mbolea ya green world
Baada ya kupita kwenye maabara za hapa nchini Tanzania, hatimaye mbolea hii imekubalika na kupewa usajili rasmi na Tanzania Fertilizer Regulatory Authority (TFRA). Mbolea hii imesajiliwa kwa jina la Nutriplant Organic Plus Fertilizer tarehe 18/09/2017 na kupewa usajili namba 0239.

 

Mbolea - green world

 

Tunawashauri watanzania kuanza kuiutumia mbolea hii kwani ina faida nyingi zaidi ya zile zinazopatikana kwenye mbolea nyingine tulizozizoea za kufukia ardhini. Faida ya zaidi ya kuongeza uwingi na ubora wa mazao yako, mbolea hii huiboresha ardhi yako badala ya kuiharibu kama ilivyo kwa mbolea nyingine.

Green World Yashiriki Maonyesho Ya 12 Ya Nchi Za Afrika Mashariki

 

Moanyesho ya rock city mall mwanza

 

Kampuni ya Green World ilishiriki maonyesho ya 12 ya nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika katika jiji la Mwanza kwenye viwanja vya Rock City Mall. Maonyesho hayo yalianza tarehe 25 Agosti 2017 na kwisha tarehe 3 Septemba 2017. Katika maonyeshio hayo, kampuni ya Green World iliweka bidhaa zake kwenye hema namba 28.

Maelfu ya wananchi wa Mwanza walipata maelezo kuhusu bidhaa za  na fursa ya biashara ya kampuni hii. Wananchi kwa ujumla walizifurahia sana bidhaa hizo na wengi walizinunua ili wakazijaribu.

Pamoja na kununua na kupata maelezo hayo, wananchi pia walipata kujua ofisi ya kampuni hii iliyopo mtaa wa Rufiji karibu kabisa na soko la Mirongo (soko la mkulima).

 

wanachi kwenye maonyesho ya rock city mall mwanza

 

Kampuni ilitunukiwa cheti kwa kushiriki na kuonyesha bidhaa bora katika maonyesho hayo.

 

Laurian.

 

Wanachama Wa Green World Washiriki Maonyesho Ya 41 Ya SabaSaba

 

 

maonyesho ya sabasaba

 

Wanachama wa kampuni ya Green World wameshiriki kwenye maonyesho ya biashara ya 41 yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Dar Es Salaam.  Maonyesho hayo yalianza tarehe 28 mwezi  Juni 2017 na kuisha tarehe 13 mwezi wa Julai 2107.

Wanachama hao walionyesha bidhaa za kampuni wakiwa ndani ya hema la Benjamin Wiliam Mkapa, chumba namba 21.

Wananchi kwa mamia kila siku walipata fursa ya kuelezwa kuhusu bidhaa za kampuni na fursa ya biashara inayotolewa na kampuni hiyo. Kwa ujumla, watu walizifurahia sana bidhaa hizo na baadhi walizinunua ili wakazijaribu. Wengi pia waliipenda fursa inayotolewa na kujiorodhesha ili waanze kupewa mafunzo mara baada ya kumaliza maonyesho.

 

sabsaba 2017

Video fupi ya maonyesho ya Green World – Sabasaba

 

Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi, wanachama hao wameamua kutoa fursa kama hiyo kwa wananchi wa Mwanza kupitia maonyesho ya 12 ya nchi za Afrika Mashariki (The 12th East Africa Trade Fair 2017) yatakayofanyika kwenye viwanja vya  Rock City Mall kuanzia tarehe 25 Agosti hadi tarehe 3 Septemba 2017.

Kwa hakika hii ni nafasi ya kipekee kwa wakazi wa Mwanza.

 

 

SEMINA YA PILI KIBAYA-KITETO

 

Kiteto may 2017

 

 

Siku ya jumamosi ya tarehe 6 Mei 2017, semina ya pili ya kampuni ya Green World ilifanyika mjini Kibaya- Kiteto. Semina hiyo iliandaliwa na wanachama wa Green World wa mjini humo, ndugu Thomas Mpalazi na Dorcas Manyama.  Maandalizi yalifanywa kwa ustadi mkubwa na mnamo saa 9.15 za alasiri, semina ilifunguliwa na ndugu Thomas Mpalazi.

Semina hiyo iliendeshwa kwa ushirikiano na wanachama wawili waliotoka Dar Es Salaam, ndugu Laurian Mwajombe na ndugu Hilda Mahende. Semina hiyo ilizungumzia umuhimu wa kulinda afya zetu kutokana na mazingira mabaya yanayotokana na uchafuzi wa mazingira na staili mpya za maisha zinazoendana na kiwango cha sayansi na teknolojia ya sasa. Semina hiyo pia ilitoa fursa kwa wananchi wa Kiteto kujiunga na kampuni ya Green World ili waweze kuboresha vipato vyao.

Kutokana na umakini wa waliohudhuria semina hiyo na kuwa na maswali mengi ya msingi, semina hiyo iliendelea hadi saa 12.30.

 

Hilda Kiteto may2017

 

Ndugu Hilda Mahende aliwasimulia washiriki historia yake ya mafanikio aliyoyapata katika kipindi cha miaka 3 toka alipojiunga, ambapo alielezea safari  mbalimali alizozipata kutokana na kampuni ya Green World na jinsi hamu yake ya kumiliki gari binafsi ilivyobarikiwa na kampuni hii.

Semina ilikuwa na mafanikio makubwa na wananchi walipata nafasi ya kununua bidhaa walizozihitaji. Wote kwa pamoja waliwashukuru waandaaji na waendeshaji wa semina na kuwaomba kuwa wawe na moyo wa kurudi mjini hapo kwa mafunzo zaidi.

 

Laurian.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Pata Mahitaji Yako Ya Dawa Za Nje Kwa Matatizo Yanayokusumbua Ukiwa Tanzania. Boresha Afya Yako Kupitia Tovuti Hii